MWANZO
Kuumbwa ulimwengu
11 Hapo mwanzo, Mungu aliumba
mbingu na dunia.« ^Dunia ilikuwa
bila umbo na tupu. Giza lilikuwa lime-
funika vilindi vya maji na roho ya
Mungu ^ ilikuwa ikitanda juu ya maji.
3 Mungu akasema, "Mwanga uwe,"
mwanga ukawa. ^ Mungu akauona mwa-
nga kuwa ni mwema. Kisha Mungu
8 Mungu akaliita anga "Mbingu." Ikawa
jioni, ikawa asubuhi; siku ya pili.
9 Mungu akasema, "Maji yaliyo chini
ya mbingu na yakusanyike mahali pamo-
ja, nchi kavu itokee." Ikawa hivyo.
1® Mungu akapaita mahali pakavu "Nchi"
na kusanyiko la maji akaliita "Bahari."
Mungu akaona kuwa ni vyema.
11 Kisha Mungu akasema, "Ardhi
na ioteshe mimea: mimea izaayo mbe-
gu, na miti izaayo matunda yenye
mbegu." Ikawa hivyo. i^Basi, ardhi
ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa
jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye
mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona
kuwa ni vyema. "i^awa jioni, ikawa
asubuhi; siku ya tatu.
14 Mungu akasema, "Mianga na
iweko angani, itenge mchana na usiku,
ionyeshe nyakati, majira, siku na miaka,
15 na ing'ae angani na kuiangazia dunia."
Ikawa hivyo. i^Basi, Mungu akafanya
mianga miwili mikubwa; ule mkubwa
utawale mchana na ule mdogo utawale
usiku; akafanya na nyota pia. ^^ Mungu
akaiweka mianga hiyo angani iiangazie
dunia, i^ipate kutawala mchana na
usiku, na kuutenga mwanga na giza.
akautenganisha mwanga na giza, ^ mwa-
nga akauita "Mchana" na giza akaliita
"Usiku." Ikawa jioni, ikawa asubuhi;
siku ya kwanza.
6 Mungu akasema, "Anga liwe kati-
kati ya maji, liyatenge maji sehemu
mbili." 7 Mungu akalifanya anga, akaya-
tenga maji yaliyo juu ya anga na yale
yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo.
Mungu akaona kuwa ni vyema. i* Ikawa
jioni, ikawa asubuhi; siku ya nne.
20 Mungu akasema, "Maji na yatoe
makundi ya viumbe hai na ndege waru-
ke angani." ^iBasi, Mungu akaumba
wanyama wakubwa sana wa baharini na
aina zote za viumbe vyote hai viendavyo
na kujaa majini; akaumba na aina zote
za ndege wote. Mungu akaona kuwa ni
vyema. 22 Mungu akavibariki, akasema,
"Zaeni, mwongezeke, myajaze maji ya
bahari; nao ndege waongezeke katika
nchi." 23 Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku
ya tano.
24 Mungu akasema, "Ardhi na itoe
aina zote za viumbe hai, wanyama wa
kufugwa, viumbe vitambaavyo na wa-
nyama wa porini wa kila aina." Ikawa
hivyo. 25 Basi, Mungu akafanya aina zote
za wanyama wa porini, wanyama wa
kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mu-
ngu akaona kuwa ni vyema.
26 Kisha Mungu akasema, "Tumfa-
nye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;
atawale samaki wa baharini, ndege wa
angani, wanyama wa kufugwa, dunia
yote na viumbe vyote vitambaavyo."
27 Basi, Mungu akaumba mtu kwa nmno
wake; naam, kwa mfano wake Mungu
« 1:1 Hapo . . . dunia: au: Hapo mwanzo, Mungu alipoziumba mbingu na dunia, 2 dunia.
* 1:2 roho ya Mungu: au: upepo mkubwa.
MWANZO 1-2
alimwumba. Aliwaumba mwanamume
na mwanamke. zsMungu akawabariki na
kuwaambia, "Zaeni mwongezeke, mkai-
jaze nchi na kuimiliki; mwatawale sama-
ki wa baharini, ndege wa angani, na kila
kiumbe hai kitembeacho duniani."
29 Kisha Mungu akasema, "Tazama,
nawapeni kila mmea duniani uzaao
mbegu, na kila mti uzaao matunda
yenye mbegu; mbegu zao au matunda
yao yatakuwa chakula chenu. ^oNao
wanyama wote duniani, ndege wote wa
angani, viumbe vyote vitambaavyo, naa-
m, kila kiumbe chenye uhai, chakula
chao kitakuwa majani yote ya mimea."
Ikawa hivyo. ^i Mungu akaona kila kitu
alichofanya kuwa ni chema kabisa.
Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya sita.
21 Hivyo ndiyyo mbingu na dunia
zilivyokamilika pamoja na vitu vyo-
te vilivyomo. 2 Siku ya saba Mungu
akawa amemaliza kazi yake yote aliyo-
fanya; siku hiyo ya saba Mungu akapu-
mzika baada ya kazi yake yote aliyofa-
nya. ^ Mungu akaibariki siku ya saba na
kuitakasa, kwa kuwa siku hiyo Mungu
alipumzika baada ya kazi yake yote ya
kuumba. * Hivyo ndivyo mbingu na
dunia zilivyoumbwa.
Bustani ya Edeni
Siku ile Mwenyezi-Mungu*^ alipoziu-
mba mbingu na dunia, ^Hapakuwa na
mimea juu ya nchi wala miti haikuwa
imechipua kwani Mwenyezi-Mungu ha-
kuwa ameinyeshea nchi mvua, wala
hapakuwa na mtu wa kuilima. *Hata
hivyo, maji yalitoka ardhini yakainywe-
sha ardhi yote. ^Basi, Mwenyezi-Mungu
akamwumba mwanamume kwa udongo,
akampulizia puani pumzi ya uhai, na
huyo mwanamume akawa kiumbe hai.
8 Kisha Mwenyezi-Mungu akapanda
bustani huko Edeni, upande wa masha-
riki, na humo akamweka huyo mwana-
mume aliyemwumba. 'Mwenyezi-Mu-
ngu akaotesha kutoka ardhini kila aina
ya miti mizuri izaayo matunda yafaayo
kwa chakula. Katikati ya bustani hiyo
kulikuwa na mti wa uhai na mti wa ujuzi
wa mema na mabaya.''
10 Kulikuwa na mto huko Edeni
uUotiririka maji na kuinywesha hiyo
bustani; kutoka huko mto huo uligawa-
nyika kuwa mito minne. "Jina la mto
wa kwanza ni Pishoni; huo waizunguka
nchi yote ya Hawila ambako kuna
dhahabu. i^ohahabu ya nchi hiyo ni
safi kabisa. Huko pia kuna marashi
yaitwayo bedola na vito viitwavyo sho-
hamu. i3jina la mto wa pili ni Gihoni;
huo waizunguka nchi yote ya Kushi.«
i*Jina la mto wa tatu ni Tigri,/ nao
watiririkia upande wa mashariki wa
nchi ya Ashuru; na jina la mto wa nne
ni Eufrate.
15 Basi, Mwenyezi-Mungu aka-
mtwaa huyo mwanamume, akamweka
katika bustani ya Edeni, ailime na
kuitunza. i« Mwenyezi-Mungu alimwa-
muru huyo mwanamume, "Waweza ku-
la matunda ya mti wowote katika
bustani; I'^lakini matunda ya mti wa
ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana
siku utakapokula matunda ya mti huo,
hakika utakufa."
18 Kisha Mwenyezi-Mungu akase-
ma, "Si vizuri huyu mwanamume kuwa
peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa
kumfaa." ^'Basi, kutoka katika udongo,
Mwenyezi-Mungu akaumba kila mnya-
ma wa porini na kila ndege wa angani,
halafu akamletea huyo mwanamume
aone atawapa majina gani; na majina
aliyowapa viumbe hao, yakawa ndiyo
majina yao. 20 Basi, huyo mwanamume
akawapa majina wanyama wote wa
kufugwa, wanyama wa porini na ndege
wote wa angani. Lakini hakupatikana
msaidizi yeyote wa kumfaa.
21 Basi, Mwenyezi-Mungu akamle-
tea huyo mwanamume usingizi mzito,
na alipokuwa usingizini, akatwaa ubavu
wake mmoja na kupafunika mahali pale
kwa nyama. 22 Na huo ubavu Mwenye-
zi-Mungu alioutoa kwa yule mwanamu-
me akaufanya kuwa mwanamke, aka-
mleta kwa huyo mwanamume. ^sNdipo
huyo mwanamume akasema,
"Naam! Huyu ni mfupa kutoka
mifupa yangu,
na nyama kutoka nyama yangu.
1:27-28 taz 5:1-2
c I'A Mwenyezi-Mungu: katika makala ya Kiebrania ni Yahweh, jina takatifu la Mungu ambalo
katika utamaduni wa Wayahudi halikutamkwa.
^ 2:9 mti wa uhai: Ufu 2:7; 22:2,14; ujuzi wa mema na mabaya; tafsiri nyingine: ujuzi wa kila kitu
(vilevile aya 17 na 3:5,22.)
< 2:13 nchi yote ya Kushi: hufikiriwa na wengine kuwa Mesopotamia. Lakini baadhi wadhani ni
sehemu ya kusini ya Misri (Sudani au Ethiopia.)
/ 2:14 Tigri: Kiebrania: mto huo ni Hidekeli.
MWANZO 2-3
Huyu ataitwa 'Mwanamke',^
kwa sababu ametolewa katika
mwanamume."
24Ndiyo maana mwanamume humwa-
cha baba yake na mama yake, akaamba-
tana na mkewe, nao wawili huwa mwili
mmoja.
25 Huyo mwanamume na mkewe wo-
te walikuwa uchi, lakini hawakuona haya.
Uasi wa binadamu
31 Nyoka alikuwa mwerevu kuliko
wanyama wote wa porini waliou-
mbwa na Mwenyezi-Mungu. Basi, nyoka
akamwambia huyo mwanamke, "Ati
Mungu alisema msile matunda ya mti
wowote bustanini?" ^ Mwanamke aka-
mjibu huyo nyoka, "Twaweza kula ma-
tunda ya mti wowote bustanini; ^ lakini
Mungu alisema, 'Msile matunda ya mti
ulio katikati ya bustani, wala msiuguse,
msije mkafa.'" ^ Nyoka akamwambia
mwanamke, "Hamtakufa! * Mungu ali-
sema hivyo kwa sababu anajua kwamba
mkila matunda ya mti huo mtafumbuli-
wa macho, nanyi mtakuwa kama Mu-
ngu, mkijua mema na mabaya."
6 Basi, mwanamke alipoona kuwa
mti huo ni mzuri kwa chakula, wavutia
macho, na kwamba wafaa kwa kupata
hekima, akachuma tunda lake, akala,
akampa na mumewe, naye pia akala.
■'Mara macho yao yakafumbuliwa, wa-
katambua kwamba wako uchi; hiyyo
wakajishonea majani ya mtini, wakajifa-
nyia mavazi ya kiunoni.
SJioni, wakati wa kupunga upepo,
huyo mwanamume na mkewe wakasikia
hatua za Mwenyezi-Mungu akitembea
bustanini, nao wakajificha kati ya miti ya
bustani, Mwenyezi-Mungu asipate ku-
waona. 'Lakini Mwenyezi-Mungu aka-
mwita huyo mwanamume, "Uko wapi?"
^•Naye akamjibu, "Nimesikia hatua zako
bustanini, nikaogopa na kujificha, maana
nilikuwa uchi." " Mwenyezi-Mungu aka-
mwuliza, "Nani aliyekuambia kwamba
uko uchi? Je, umekula tunda la mti
nililokuamuru usile?" ^^Huyo mwana-
mume akajibu, "Mwanamke uliyenipa
akae pamoja nami ndiye aliyenipa tunda
la mti huo, nami nikala."
13 Hapo Mwenyezi-Mungu akamwu-
liza huyo mwanamke, "Umefanya nini
wewe? Mwanamke akamjibu, "Nyoka
alinidanganya, nami nikala."
Adhabu
14 Kisha Mwenyezi-Mungu akamwa-
mbia nyoka,
"Kwa kuwa umefanya hivyo,
umelaaniwa kuliko wanyama wote
wa kufugwa,
na kuliko wanyama wote wa
porini.
Kwa tumbo lako utatambaa,
na kula mavumbi siku zote za
maisha yako.
1* Nitaweka uadui kati yako na
huyo mwanamke,
kati ya uzao wako na uzao wake;
yeye atakiponda kichwa chako,
nawe utamwuma kisigino chake."
16 Kisha akamwambia mwanamke,
"Nitakuzidishia uchungu wa kuzaa,
kwa uchungu utazaa watoto;
utakuwa na hamu na mumeo,
naye atakutawala."
17 Kisha akamwambia huyo mwana-
mume,
"Kwa kuwa wewe umemsikiliza
mkeo,
ukala matunda ya mti ambayo
nilikuamuru usile;
kwa hiyo, kwa kosa lako ardhi
imelaaniwa.
Kwa jasho utajipatia humo riziki
yako,
siku zote za maisha yako.
18 Ardhi itakuzalia miiba na magugu,
nawe itakubidi kula majani ya
shambani.
1' Kwa jasho lako utajipatia chakula,
mpaka utakaporudi udongoni
ulimotwaliwa;
maana wewe ni mavumbi, na
mavumbini utarudi."
20 Adamu* akampa mkewe jina "Ha-
wa",' kwani alikuwa mama wa binadamu
wote 21 Mwenyezi-Mungu akawatengene-
zea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi,
akawavika.
Adamu na Hawa
wanafukuzwa bustanini
22 Kisha Mwenyezi-Mungu akasema,
"Sasa, binadamu amekuwa kama nmioja
wetu, anajua mema na mabaya. Lazima
kumzuia kula lile tunda la mti wa uhai,
kwani akilila ataishi milele!" ^agasj^
Mwenyezi-Mungu akamfukuza Adamu
nje ya bustani ya Edeni, ili akailime ardhi
g 2:23 Kiebrania: maneno mwanamume . . . mwanamke; "ishi, isha" yanafanana.
^ 3:20 Adamu: Kiebrania maana yake ni "mtu".
' 3:20 Hawa: Kiebrania lalingana na neno lenye maana "uhai".
MWANZO 3-5
ambamo alitwaliwa. 24 Alimfukuza nje, na
loiweka mlinzi> upande wa masharud wa
bustani ya Edeni na upanga wa moto
uliogeuka huko na huko, kuilinda njia
iendayo kwenye mti wa uhai.
atalipizwa mara saba." Basi, Mwenyezi-
Mungu akamtia Kaini alama ya tahadha-
ri, ill yeyote atakayemwona asimwue.
i^Kisha Kaini akaondoka mbele ya Mwe-
nyezi-Mungu, akawa anaishi katika nchi
ya Ncxii,' upande wa mashariki wa Edeni.
The Bible with Deuterocanonicals in current Kiswahili
An Interconfessional Translation published as
BIBLIA
Yenye Vitabu vya Deuterokanoni
HABARI NJEMA
Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa
Published by
The Bible Society of Kenya
P.O. Box 72983
NAIROBI, Kenya
and
The Bible Society of Tanzania
P.O. Box 175
DODOMA, Tanzania
© The Bible Society of Kenya, 1995
© The Bible Society of Tanzania, 1995
Illustrations by Horace Knowles
© The British and Foreign Bible Societ
London, England, 1954, 1967, 1972.
All Rights Reserved
First Published 1995
ISBN 9966 - 40 - 592 - 5 - CLDC053P - 40M
ISBN 9966 - 40 - 593 - 3 - CLDC057P - 0.5M
KISWAHILI BIBLE DC EDITION UBS-EPF 40.5M 199'
BIBLIA
Yenye Vitabu vya Deuterokanoni
HABARI NJEMA
TAFSIRI YA USHIRIKIANO WA MAKANISA
VYAMA VYA BIBLIA
KENYA NA TANZANIA
NAIROBI : DODOMA
Eunice V. Pike Library
SUMMER INSTITUTE OF LINGUISTICS
Dallas, Texas
Given by:
BIBLE TPANSLATION
AND LITERACY:
THE NBTO OF KENYA